Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria ametahadharisha kwamba Libya inaweza kua tishio, kwa bara zima la Afrika.
Rais wa Nigeria amesema hali ya kusini mwa Libya haidhibitiki, na kwamba nchi imekua soko kubwa la silaha, jambo ambalo amesisitiza kua inahatarisha usalama wa Nigeria, na nchi nyingine za Afrika.
Buhari amesisitiza kua hatua zinapaswa kuchukuliwa kwa ajili ya kukomesha mgogoro wa ndani nchini Libya, na ameitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua za dharura, katika kukomesha machafuko ya ndani nchini humo.
Libya ilitumbukia katika machafuko ya ndani mnamo mwaka 2011, baada ya kuondolewa madarakani aliyekua Rais wa nchi hiyo, Kanali Muammar Gaddafi.
Baadhi ya maeneo ya Libya kwa sasa yanadhibitiwa na kundi la Daesh, ambalo limeyatumia vibaya machafuko ya ndani, kuimarisah udhibiti wake nchini humo
No comments :
Post a Comment