Ndege moja iliyokuwa ikibeba abiria 74 ilitua kwa dharura kwenye uwanja wa ndege wa Mogadishu baada ya mlipuko kutokea ndani ya ndege hiyo.
Shirika la habari la AP la Marekani limesema, ndege hiyo aina ya Airbus A321 ya shirika la ndege la Daallo ilikuwa inasafiri kutoka Mogadishu kwenda Djibout.
Ofisa mmoja wa Somalia anasema, watu wawili wamejeruhiwa katika ajali hiyo. Wataalamu wanaona kuwa, huenda mlipuko huo uliotomboa sehemu kubwa ya bodi la ndege hiyo ulisababishwa na kifaa cha kilipuzi
No comments :
Post a Comment