Sunday, January 10, 2016

Muuzaji dawa za kulevya duniani ‘El Chapo’ akamatwa Mexico



Muuzaji dawa za kulevya wa Mexico aliyekamatwa Joaquim “El Chapo” Guzman amerudisha katika gereza lenye ulinzi mkali ambako alitoroka miezi sita iliyopita.
Alikamatwa huku akiburuzwa na kurekodiwa na kamera wakati akipandishwa kwenye helikopta ya jeshi kupelekwa kwenye gereza la Altiplano lililopo katikati ya Mexico.
Alitoroka gerezani mwezi Julai kupitia shimo alilolichimbia chooni
Guzman alikamatwa katika mji wa Los Moschis nyumbani katika jimbo la Sinaloa – ambako alirudi kuendelea na shughuli zake za dawa za kulevya.
Wakati wa shambulizi hilo la asubuhi siku ya Ijumaa, aliweza kutoroka kupitia bomba lakini baadae alikamatwa na wanajeshi baada ya kufyatuliana risasi.


No comments :