Kwenye mechi hiyo Luca Zidane alitolewa nje kwenye mechi hiyo kwa kosa
la kumkwatua mchezaji mwenzake, lakini pia kabla hajapewa kadi hiyo
alileta ubabe wa kumvimbia mwenzake kwa kusukumana kwa kichwa kama Mbuzi
wanavyofanyaga
Luca Zidane ambae ni goli kipa wa club ya Real Madrid kwenye kikosi cha under 17 amepewa kadi nyekundu kwenye mechi dhidi ya wapinzani wao Atletico Madrid.
Luca Zidane (katikati) alionekana akimpiga kichwa mchezaji wa Atletico Madrid
Dogo huyu ameingia kwenye vichwa vya habari baada ya kitendo hicho kufananishwa na baba yake ambae aliwai kumpiga kichwa Marco Matellazi kwenye fainali za Kombe la Dunia mwaka 2006
Zidane ana watoto wa 4 ambapo Enzo mkubwa ni captain wa Real Madrid B,
Luca anacheza kwenye kikosi cha under 17 na Theo na Elyaz wanacheza
kwenye Academy
No comments :
Post a Comment