Monday, January 11, 2016

Messi anaweza kunyakuwa Ballon d’Or ya tano kwa sababu hizi


Lionel Messi amenyakuwa Balon d’Or nne
Orodha fupi ya watu watatu ilitoka kwenye majina 23, na mshindi atatangazwa katika sherehe za Tuzo ya Mpira wa Dhahabu ya FIFA (Ballon d’Or) mjini Zurich Januari 11.
Mchambuzi wa soka Mhispania Guillem Balague, anachambua wawaniaji hao watatu.
Messi amenyakuwa tuzo hiyo mara nne na pia anatabiriwa na Sky Bet kushinda tuzo hiyo kwa mara ya tano, akiwa ameikosa mara mbili ikichukuliwa na Cristiano Ronaldo.




Ronaldo, Messi na Neymar wanawania tuzo hiyo leo jijini Zurich, Uswisi

Ronaldo, Messi na Neymar wanawania tuzo hiyo leo jijini Zurich, Uswisi
Ronaldo, Messi na Neymar wanawania tuzo hiyo leo jijini Zurich, Uswisi
Sababu hizi zinamfanya Messi aweze kunyakuwa tuzo hiyo leo usiku;
Kwanza, aliiongoza Barcelona kunyakuwa La Liga, Ligi Kuu ya Mabingwa Ulaya na Copa de Rel msimu uliopita. Alifunga magoli 28 katika mzunguko wa pili wa msimu.
Alishindwa kuing’arisha nchi yake kwenye Copa America nchini Chile majira ya joto, lakini amerudi kwenye ubora wake akitokea majeruhi mwezi huu na Balague anafikiria kuwa anastahili kunyakua tuzo hiyo
.Ronaldo anawania tuzo hiyo kwa mara ya tatu mfululizo
Ronaldo anawania tuzo hiyo kwa mara ya tatu mfululizo
Ronaldo anawania tuzo hiyo kwa mara ya tatu mfululizo
Kwa upande wa Ronaldo ambaye anadhamiria kunyakuwa tuzo hiyo kwa mara ya tatu mfululizo tangu 2013 na 2014, japokuwa ana kazi ya ziada baada ya kumaliza msimu uliopita bila hata medali ya fedha. Alifunga magoli 29 katika mzunguko wa pili wa 2014/15 na kuwa mfungaji wa muda wote Real Madrid mwezi Oktoba, lakini uchezaji msimu huu umekuwa na walakini.
“Motisha wa Ronaldo kwenye mechi umekwisha, hakuna shaka juu ya hilo,” Balague aliiambia Sky Sports. “Real Madrid bora ilimalizika mwezi Desemba baada ya Kombe la Dunia la Vilabu na ushindi wa mechi 22 mfululizo. Baada ya hapo, kwa mujibu wa Rais wa Real Madrid Florentino Perez mwenyewe, timu ilioza. Hilo lilimuathiri kila mtu, hususani Ronaldo.”
Neymar anapewa nafasi kubwa ya kumpiku Ronaldo leo
Neymar anapewa nafasi kubwa ya kumpiku Ronaldo leo
Neymar anapewa nafasi kubwa ya kumpiku Ronaldo leo
Neymar alifunga magoli 24 katika mzunguko wa pili Barcelona iliposhinda mataji matatu msimu wa 2014/15, na kumfanya awe mchezaji mmarufu wakati akiwa nje majeruhi. Raia huyo Brazil anaungana na chati ya wafungaji Hispania akiwa na magoli 15 msimu huu La Liga, huku Sky Bet ikimuweka nafasi ya tatu kushinda tuzo, Balague anafikiria kuwa anaweza kumpiku Ronaldo.
Unafikiri nani atanyakuwa tuzo hiyo mjini Zurich, Uswisi?

No comments :