Celine Dion hatarejea kwenye makazi yake mjini Las Vegas hadi Februari kufuatia kifo cha mume wake Rene Angelil, ambaye amefariki kutokana na saratani siku ya Alhamisi akiwa na miaka 73.
Muimbaji huyo, 47, alikatisha tamasha lake haraka la kwenye The Colosseum huko Caesars Palace siku ya Jumamosi na Jumapili na kutoa taarifa rasmi akithibitisha hatarudi hadi Februari 23.
Celine na Rene walitimiza miaka 21 ya ndoa yao Desemba 17, 2015
Angelil, ambaye alipambana na saratani kwa miaka 20, alifariki akiwa nyumbani Vegas siku mbili baada ya kusherehekea miaka 74 ya kuzaliwa kwake na mwezi mmoja baada ya kutimiza miaka 21 ya ndoa yao Desemba 17.
Rene Angelil alianza kumsimamia Celine kimuziki akiwa na miaka 12
Katika ujumbe alioutuma kwenye ukurasa wake wa Facebook, Dion alisema, “mumewe mpendwa alipambana vikali na saratani. Familia inapenda kuomboleza kwa faragha.”
Wakiwa na watoto wao Eddy na Nelson
Mshindi mara tano wa Grammy alikuwa na miaka 12 wakati Rene mtalaka mara mbili alipomtangaza kuwa nyota na kuamua kuwa meneja na mshauri wake.
No comments :
Post a Comment