Wednesday, June 4, 2014
SIKU NANE KABLA YA KOMBE LA DUNIA
Je wajua kwamba... Ili kuhakikisha usalama wa watu wengi watakaokwenda Brazil kutazama mechi, ndege zisizo na rubani zitatumika kufanya doria. Ndege hizo - drones- aina ya PackBot 510 hutumiwa na jeshi la M...arekani. Zinaweza kuongozwa kutoka mbali na huweza kung'amua vitu vya hatari au kwenda sehemu za hatari. Mbali na ndege hizo pamoja na maroboti ya Kimarekani kulinda usalama, miwani zenye camera zinazoweza kutambua sura za watu pamoja na vifaa vyenye teknolojia ya kisasa vitatumika kulinda usalama wa raia na watalii. Wanajeshi wa Brazil ndio watakuwa wakilinda usalama katika miji ambayo mechi zitachezwa
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment