Monday, June 2, 2014

MFALME WA SPAIN KUACHIA NGAZI


Mfalme wa Spain Juan Carlos ameamua kung'atuka. Tangazo hilo limetolewa na Waziri Mkuu, Mariano Rajoy.
Mfalme Juan Carlos mwenye umri wa miaka 76 ametawala Hispania tangu mwaka 1975. Mtoto wake, Mwanamfalme Filipe, 45, atachukua madaraka hayo ya Ufalme.
Katika muda mwingi wa utawala wake, Juan Carlos alikuwa mmoja wa watawala maarufu wa kifalme.
Hata hivyo hivi karibuni wananchi wengi wa Spain wamepoteza imani naye, hasa kutokana na uchunguzi wa muda mrefu wa ufisadi dhidi ya mwanae wa kike na mumewe

No comments :