Wednesday, June 4, 2014
Abdul Fattah al-Sisi ndiye rais mpya wa Misri
Wafuasi wa Rais Abdul Fattah al-Sisi wakishangilia ushindi huo wa uchaguzi huo wiki iliyopita. Wamisri wengi wanaamini kuwa Sisi ndio mkombozi wao baada ya miata mitatu ya ghasia.
Andul Fattah al-Sisi amewataka Wamisri kufanya kazi ili kurudisha hali ya usalama baada ya kutangazwa kuwa ndiye mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika wiki iliyopita.
Mkuu huyo wa majeshi wa zamani alisema anataka ‘ukombozi’ na ‘haki kwa jamii’, akifuata sera ya mapinduzi ya mwaka 2011.
Sisi alizungumza baada ya maafisa wa uchaguzi kutangaza kwamba alipata asilimia 96.9 ya kura huku mpinzani wake mmoja, mwenye siasa za mrengo wa kushoto Hamdeen Sabahi akiambulia asilimia 3.1 ya kura
Komandoo huyo mstaafu alimpindua Rais Mohammed Mosrsi mwezi Julai, 2013.
Amekuwa katika mapambano na chama cha Morsi cha Muslim Brotherhood, ambao waliugomea uchaguzi waliouita “uchaguzi wa damu”.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment