Saturday, May 31, 2014
Kituo cha daladala Mwenge kufungwa rasmi kesho
Moja ya daladala ya Mwenge-Kariakoo ikiwa katika kituo cha daladala cha Mwenge ambacho kuanzia Jumatatu, mabasi yote yanapita kituoni hapo yatahamia kituo cha Makumbusho.
Mamlaka ya Udhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu (SUMATRA) inawataarifu wamiliki, madereva na abiria wote kuwa kituo cha daladala cha Mwenge kitafungwa kesho, siku ya Jumapili (Juni1). Hivyo basi, kituo kitakachotumika kuanzia siku ya Jumatatu ni kituo cha Makumbusho tu.
Mamlaka hiyo ya usafiri imeeleza sababu za kufungwa kwa kituo hicho kuwa ni kwa sababu ya ufinyu wa eneo hilo na hivyo kusababisha daladala kushindwa kuingia kituoni kwa wakati hasa nyakati za asubuhi na jioni na hivyo kusababisha msongamano kwenye kituo hicho.
Kwa mujibu wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kituo eneo hilo litabakia kuwa la wazi.
Pia mamlaka imewataka madereva na abiria kuzingatia agizo hilo na kudai sheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayekiuk
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment