Saturday, March 12, 2016

Maalim Seif afichua alichozungumza na Dkt. Magufuli, Dkt. Shein

                                                        Maalim Seif Shariff Hamad akiwa na Rais John Magufuli
Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amesisitiza kuwa hali yake imezidi kuimarika kwani maumivu aliyokuwa akiyasikia yamepungua huku akisisitiza kuwa hajazungumza masuala ya kisiasa na wageni waliomtembelea.
Amesema hajazungumza masuala ya Uchaguzi Mkuu Zanzibar na Rais John Magufuli wala Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, waliomtembelea kwa ajili ya kumjulia hali.

             Maalim Seif Shariff Hamad akisalimiana na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein
Maalim Self aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati alipotembelewa na Waziri Mkuu Mstaafu, ambaye pia alikuwa mgombea Urais kwa tiketi ya Chadema, anayeungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) Edward Lowassa, ambaye alikwenda kumtembelea hotelini anakopumzika.
“Nataka kuwahakikishia kuwa hali yangu ni nzuri na kwa sasa nipo hapa kwa kuwa madakatari wameniambia nipumzike, wageni wangu walikuja kunijulia hali tu na hatujazungumza masuala yoyote ya ya kisiasa wala Uchaguzi wa Zanzibar,” alisema.

No comments :