Friday, March 4, 2016

Barcelona yavunja rekodi ya miaka 27

                                            Lionel Messi alifunga magoli matatu katika mechi hiyo
Barcelona imevunja rekodi ya miaka 27 Hispani kwa kushinda mechi 35 mfululizo katika mashindano yote msimu huu baada ya kuinyka Rayo Vallecano.
Lionel Messi alifunga magoli matatu kufuatia wenyeji kusambaratika baada ya Ivan Rakitic kufunga goli la kwanza, kutokana na makosa ya mlinda mlango.
                      Ivan Rakitic akishangilia goli lake la kwanza dhidi ya Rayo Vallecano
Diego Llorente alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya Ivan Rakitic.
Barcelona ilishinda magoli 5-1 dhidi ya Rayo Vallecano. Goli la tano lilifungwa na Arda Turan.
Lionel Messi alifunga magoli matatu katika mechi hiyo
                   Timu ya Luis Enrique kwa sasa iko juu alama nane ikifuatiwa na Atletico.
Msimamo wa Ligi Kuu Hispania
Msimamo wa Ligi Kuu Hispania


No comments :