Tuesday, May 26, 2015

Carlo Ancelotti atupiwa virago Real Madrid

Kocha Carlo Ancelotti ametimuliwa Real Madrid
Kocha Carlo Ancelotti ametimuliwa Real Madrid
Real Madrid wamemfukuza Carlo Ancelotti ikiwa ni mwaka na siku moja tangu ashinde taji la 10 Kombe la Ulaya.
Florentino Perez alithibitisha mbele ya waandishi wa habari Jumatatu usiku kuhusu uamuzi huo wa kumfukuza kocha huyo wa tisa katika miaka yake 12 akiwa kama rais wa klabu hiyo, lakini hakumtaja Rafa Benitez kama kocha mpya wa klabu hiyo.
Carlo Ancelotti ni kocha wa tisa kutimuliwa na rais  Florentino Perez
Carlo Ancelotti ni kocha wa tisa kutimuliwa na rais Florentino Perez
Kocha huyo wa zamani wa Liverpool anatazamiwa kuchukuwa nafasi hiyto lakini habari za kufukuzwa kwa Ancelotti hazijapokelewa vizuri na wachezaji na mashabiki
Idadi ya makocha waliowahi kufukuzwa na rais Perez
Vicente del Bosque (June 23, 2003)
Carlos Queiroz (May 24, 2004)
Jose Antonio Camacho (Sep 20, 2004)
Marino Garia Remon (Dec 30, 2004)
Vanderlei Luxemburgo (Dec 4, 2005)
Fabio Capello (June 28, 2007)
Bernd Schuster (Dec 9, 2008)
Manuel Pellegrini (May 26, 2010)
Carlo Ancelotti (May 25, 2014)
Florentino Perez alithibitisha kumtimua kocha wa tisa katika miaka yake 12 akiwa kama rais Real Madrid
Florentino Perez alithibitisha kumtimua kocha wa tisa katika miaka yake 12 akiwa kama rais Real Madrid

No comments :