Saturday, October 4, 2014

PRESENTERS WENGI WANASHINDWA KUTOFAUTISHA HATWATU WA KUWASHINDANISHA BELLA 9 NOT THAT FAR TO R&B, WHILE DIAMOND HE IS DOING AFROPOP THE STYLE THAT GOT DIFFERENTFUSSION OF AFRICAN INSTRUMENT. SOMA HII INTERVIEW NILIYOIKUTA KTK UKURASA MMOJA WA MTANDAO







SWALI LILIKUWA JEE BELLA 9 UNAWEZA KUFANYA KZAI NA DIAMOND??????



Msanii wa bongo fleva kutoka Mkoani Morogoro, Belle 9 amesema kwa sasa hafikirii kufanya collabo na Diamond Platinumz kwa kuwa bado haoni chemistry (muendano sawa) kati yao.
Akiongea katika Exclusive Friday ya kipindi cha Sunrise cha 100.5 Times Fm, Belle 9 amesema haoni kama kuna chemistry kati yake na mwimbaji huyo ingawa haweki mipaka ya collabo kati yao.
“Kama ikitokea nina wimbo ambao yeye anaweza kuplay part yake vizuri tunaweza tukafanya. Ikitokea mimi nimeandika wimbo ambao nahisi kabisa yeye akikaa atafit tunaweza tukafanya. Lakini sio chemistry hapo kwanza.”
Mwimbaji huyo amesema hivi sasa anafikiria kufanya kazi na mzee Zahir Zorro au Banza Stone kwa ajili ya kupata kitu cha kipekee.
“Hawa vijana wanaimba vizuri. Kiwango kipo, sijasema sioni… lakini the same. Mimi ninahitaji kitu unique kwa sababu nahisi kwa kumshirikisha Zahir au Banza Stone hivi…yaani watu ambao mimi naweza kuchukua kitu pale. Kuna watu wengi ambao naweza kujifunza vitu vingi.” Belle 9 amefafanua.
Hata hivyo, amesema wasanii wapya wa kizazi kipya wanafanya vizuri sana pia na akawataja wengi aliowashirikisha kwenye nyimbo zao kuonesha jinsi anavyowakubali.




No comments :